Zahera alikuwa tayari kuwalipa wachezaji, mgomo wamsikitisha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Apr 2019
Zahera alikuwa tayari kuwalipa wachezaji, mgomo wamsikitisha

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameeleza kusikitishwa na kitendo cha wachezaji wa timu hiyo kugomea mazoezi leo asubuhi huku wakifanya tukio hilo bila ya kumshirikisha

Zahera amesema hakutarajia mgomo hasa ukizingatia muda uliobaki ni mdogo ligi kumalizika

Aidha kocha huyo raia wa DR Congo amebainisha kuwa kama wachezaji wangemshirikisha angeweza hata kuwalipa fedha yeye mwenyewe wakati wakisubiri kukamilishwa kwa stahiki zao

"Ni kweli wachezaji leo waligomea mazoezi, inanishangaza sana wamegoma kisa tuna matatizo ya mishahara na bonus"

"Leo tukiwa tunajiandaa kuanza mazoezi niliwaambia sasa hivi nawapigia viongozi simu ili kesho waje wote mazoezini waonane na wachezaji"

"Wachezaji wakasema kuwa viongozi hawatofika, nikawahakikishia wachezaji wangu kuwa kesho viongozi watafika na endapo wasipofika basi keshokutwa wao watakuwa huru kufanya kilicho sahihi kwao"

"Wachezaji wote walikuwa wamekaa ng'ambo ya pili, mimi napiga filimbi waje nawaona Juma Abdul na Ajib wanavuka uwanja wanaenda ng'ambo wakaungana na wachezaji wengine.

"Mimi nawaita wao kumbe wanafanya kikao mara nasikia aaah tusiende bana kocha atatuambia hivi na vile"

"Kisha wakaanza kupanda magari yao wengine wakapanda pikipiki na kuondoka"

"Saa nne na nusu viongozi wakafika! na kesho kama kuna mchezaji hatofika basi asahau kuichezea tena Yanga"

"Kama wangenishirikisha ningekuwa tayari nikachukue hela zangu Congo niwape ila wamefanya vitu ya ovyo sana"

"Kila kitu wanakifahamu na haya matatizo ni toka mwaka jana mwezi wa sita yapo na wanaona jitihada za kujikwamua zinafanyika tatizo kubwa wachezaji wengi hawana malengo ya mbali kisoka"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’