Klabu ya Simba inaongoza kwa kuzawadiwa mikwaju ya penati ligi kuu ya Tanzania Bara msimu huu
Mpaka sasa Simba imezawadiwa jumla ya mikwaju tisa ya penati
Leo katika mchezo dhidi ya KMC, Simba ilizawadiwa mikwaju miwili ambapo ilifanikiwa kufunga mmoja uliowapa ushindi wa mabao 2-1
Gumzo kubwa lililojiri baada ya mchezo huo ni jinsi waamuzi 'walivyoinyonga' KMC na kuipendelea Simba hali iliyoibua malalamiko miongoni mwa mashabiki wa soka
Ukiachilia malalamiko ya ratiba, msimu huu waamuzi wamechangia kwa kiasi kikubwa kuharibu radha ya ligi na kuondoa ushindani uliokuwa ukitarajiwa
ADVERTISE HERE