Aliyekuwa mlinda lango wa Yanga Beno Kakolanya ambaye kwa sasa yuko nje ya klabu hiyo kutokana na mgogoro uliopo, amesema hana kinyongo na Yanga kwani ilimvumilia kwa karibu msimu mzima wakati akisumbuliwa na tatizo la goti
Kakolanya aliyeomba kuvunjwa kwa mkataba wake na Yanga, amesema kilichotokea na kumfanya ajiweke pembeni ni kukiukwa kwa makubaliano ya mkataba
Amesema kama mabosi wa Yanga watakaochaguliwa watataka kumrejesha katika kikosi hicho yupo tayari kurejea lakini kwa makubaliano maalumu.
"Siwezi kukataa kwasababu naamini kabisa sina tatizo nao, bali waweke pesa mezani nitasaini na kuendelea na kazi yangu kama kawaida, inabidi itambulike mpira ni kazi kama kazi zingine," amesema
Kakolanya amepeleka barua Kamati ya TFF ya Sheria na Hadhi za Wachezaji akiomba aachwe huru na Yanga baada kile alichokileleza kukiukwa kwa makubaliano ya mkataba
Suala lake linasubiri kutatuliwa na Kamati hiyo
Klabu ya Yanga inatarajiwa kufanya uchaguzi wa kuwapa viongozi wapya May 05 2019