Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema timu hiyo imejipanga kuwaadhibu vikali Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa Jumatatu ijayo kwenye uwanja wa Taifa
Mchezo huo ambao Yanga itakuwa ugenini, unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka kwani unaweza kutoa taswira ya hatma ya ubingwa kwa timu hizo zinazofuatana kwenye msimamo wa ligi kwa muda mrefu
Katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram Ten ameandika;
"Yanga Africans Football Club , mabingwa mara 27 katika ligi kuu bara ,msimu wetu wa 2018/2019 tumecheza jumla ya mechi 32 ,tumeshinda mechi 23 ,tumetoka sale mechi 5 ,tumepoteza mechi 4 .
Tumefunga jumla ya magoli 51 na kufungwa jumla ya magoli 22 na kuweza kufanikisha jumla ya point 74
Msimu huu tumecheza mechi 16 nyumbani,na kushinda mechi 14 ,tumetoka sale mechi 1 ,tumefungwa mechi 1 nyumbani ,temefunga jumla ya magoli 34 na kufungwa magoli 13 pekee na kukusanya jumla ya point 43 kwa mechi za nyumbani.
Mechi za ugenini ,tumecheza mechi 13 ,tumeshinda mechi 10 ,tumetoka sale mechi 1 ,tumepoteza mechi 3,tumefunga jumla ya magoli 27 na kufungwa jumla ya magoli 7 na kukusanya point 31.
Tarehe 29 .04.2019 tutakuwa na mechi dhidi ya Azam ,na tutakuwa mgeni wa Azam, tutarajie soka la anasa kutoka Yanga Africans ,huku tukiongozwa na ncha yetu Kali ya kufunga magoli Heritier Makambo na yake style ya kushangilia ya ,"Make It Clap" "
