Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Malangwe Mchungahella amesema wagombea walioenguliwa kutokana na mapingamizi, wanaweza kukata rufaa kuanzia kesho Jumatano hadi Ijumaa
Mchungahella ambaye Kamati yake inashirikiana na Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kusimamia uchaguzi huo, amesema rufaa hizo zitasikilizwa na Kamati ya Rufani ya uchaguzi ya TFF
Miongoni mwa wagombea walioenguliwa ni aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti Samwel Lukumay alikuwa anawania nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Wajumbe Hussein Nyika, Siza Lymo na Thobias Lingalangala
Baada ya rufaa hizo kusikilizwa, orodha ya mwisho ya wagombea inatarajiwa kutangazwa Jumatatu ijayo tayari kwa kuanza mchakato wa kapeni siku ya Jumanne April 30
Uchaguzi utafanyika May 05