Namungo Fc jana ilikuwa timu ya kwanza kujihakikishia kupanda daraja ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuifunga Mawenzi Market ya mkoani Morogoro kwa mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa jamhuri
Timu hiyo inayodhaminiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, imekuwa na msimu mzuri katika ligi daraja la kwanza ikiwa imepoteza mchezo mmoja tu. Imepanda daraja huku ikiwa na alama 40 na michezo miwili kibindoni
Namungo inayonolewa na Hitimana Thiery anayesaidiwa na beki wa zamani wa Yanga Bakari Malima, pia ilifanya vizuri kwenye michuano ya kombe la FA (ASFC) ambapo ilitolewa na Yanga kwenye hatua ya 16 bora
ADVERTISE HERE