Tulishamuondoa Beno kwenye mipango yetu - Kaya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Apr 2019
Tulishamuondoa Beno kwenye mipango yetu - Kaya

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaya amesema mlinda lango Beno Kakolanya alishaondolewa kwenye mipango ya Yanga na suala lake liko katika hatua za kumalizwa kisheria

Kaya amesema baada taratibu zote za kishasheria kukamilishwa, Beno atakuwa huru kuendelea na maisha yake ya soka mahali pengine

"Suala la Beno lipo katika sheria zaidi, Yanga na Beno walishaachana kwa sababu angekuwa bado anahitajiwa kufanya kazi Yanga sidhani mpaka leo kama angekuwa nje ya timu," Kaya ameiambia UFM

"Sidhani kama ni sawa kulizungumzia suala ambalo tayari limeshapita"

"Taratibu nyingine za kumalizana zipo nyuma ya pazia tutamalizana na ataendelea na maisha yake kama ambavyo sasa hivi anavyoendelea na maisha yake na Yanga inaendelea na maisha yake"

Beno aliondolewa kikosini mwishoni mwa mwaka jana baada ya kufanya mgomo uliosababisha mgogoro baina yake na kocha Mwinyi Zahera

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’