Zahera azipigia hesabu Azam Fc, Lipuli Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Apr 2019
Zahera azipigia hesabu Azam Fc, Lipuli Fc

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema licha ya changamoto za waamuzi wanazokabiliana nazo kwenye ligi, hawatakata tamaa na watafanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo unaofuata dhidi ya Azam Fc utakaopigwa uwanja wa Taifa April 29 2019

Yanga imesalia na michezo sita kumaliza msimu huku imchezo mmoja dhidi ya Biashara United ukitarajiwa kupigwa nje ya Dar

Yanga itarejea jijini Dar es salaam kutumia uwanja wa Taifa baada ya kumalizika fainali za AFCON U17 April 28 2019

Zahera amesema watahakikisha wanashinda michezo yote iliyobaki pamoja na kuweka msisitizo zaidi kwenye michuano ya kombe la FA (ASFC) wakitarajia kucheza na Lipuli Fc mwanzoni mwa mwezi wa tano katika mchezo wa nusu fainali

"Unajua mimi nimezunguka nchi nyingi sana Afrika lakini sijawahi kuona maamuzi ya hovyo kama ya waamuzi wa Ligi ya Tanzania, Hakuna haki na kungekuwa na haki nina uhakika sasaivi tungekuwa tushajihakikishia ubingwa"

"Kwa sasa tumesahau yote, tunajipanga kuelekea michezo inayofuata ukiwemo wa Azam Fc ili kuhakikisha tunashinda mechi zote zilizosalia huku tukihakikisha tunatwaa ubingwa wa Kombe la ASFC ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’