Bodi ya ligi yatahadharishwa mechi za saa nane

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Apr 2019
Bodi ya ligi yatahadharishwa mechi za saa nane

Mtaalamu wa misuli ya mwili wa binadamu Dk Kitambi Mganga ameishauri Bodi ya ligi kuu kuwa makini na utaratibu wa kupanga michezo ya ligi kuu saa nane mchana wakati wa jua kali

Dk Mganga amesema kitaalam, muda huo sio mzuri kwani unaweza ukasababisha madhara makubwa kwa wachezaji yakiwemo matukio ya vifo

"Wachezaji wanapocheza wakati wa jua kali wanakuwa katika hali ya kukausha maji mwilini kwa haraka na hivyo kuwepo na hatari ya kupatwa na shambulio la moyo au kuziba moyo na misuli kukakamaa," amesema

"Shambulio la moyo linatokana na mwili kulazimishwa kufanya kazi ngumu wakati wa jua kali, moyo unaziba, ulimi unatoka nje, misuri inashindwa kufanya kazi ni hatari kubwa mchezaji anaweza kupoteza maisha uwanjani kama hakutakuwa na mtaalamu mwenye kujua atoe huduma gani"

Dk Mganga ambaye ni Daktari wa Coastal Union, amesema kama kuna ulazima wa kuchezesha mechi hizo katika muda huo basi mwamuzi anaweza kutenga hata dakika moja ya kuwapa nafasi wachezaji kunywa maji utaratibu ambao hutumika kote duniani ambapo mchezo husimamishwa kwenye dakika ya 25-30 kuwapa nafasi wachezaji kunywa maji

Msimu huu baadhi ya michezo ya ligi kuu imekuwa ikipigwa saa nane mchana ili kutoa nafasi kwa michezo mingi kuonyeshwa 'mbashara' na Azam TV

Michezo ya ligi iliyopigwa jana ambayo ilihusisha Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga na Coastal Union dhidi ya Simba, ilipigwa saa nane mchana ili kuepusha muingiliano wa ratiba na michuano ya AFCON U17 inayoendelea jijini Dar es salaam

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
16h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
17h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
17h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’