Mchakato wa uchaguzi Yanga unazidi kushika kasi ambapo leo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF Malangwe Mchungahela ambaye Kamati yake inashirikiana na Kamati ya uchaguzi iliyoundwa na Yanga, ametangaza kuondolewa kwa baadhi ya wagombea ambao walikuwa wamewekewa mapingamizi
Akizungumza na Wanahabari Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Mchungahela amesema waliokuwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji uongozi uliopita ambao wamejitosa kuwania uongozi tena, Hussein Nyika, Thobias Lingalangala, Samwel Lukumay na Siza Lymo wameondolewa kwenye mchakato huo baada ya kuwekewa mapingamizi
Mchungahella amesema kwa pamoja wagombea hao walishindwa kuwasilisha taarifa za mapato na matumizi katika kipindi chao kilichopita.
Taarifa kamili ya wagombea


ADVERTISE HERE