Mshambuliaji Erick Msagati aliyepandishwa kutoka Yanga B leo amepata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar
Msagati alipandishwa timu ya wakubwa baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi iliyofanyika mapema mwaka huu visiwani Zanzibar
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amejipambanua kwa kuwaamini vijana ambapo atakuwa mchezaji wa nne kuitumikia timu ya wakubwa msimu huu
Paulo Godfey 'Boxer', Cleofas Sospeter na Gustava Simon wote wamepata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza baada ya kupandishwa kutoka Yanga B
Boxer amejihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza wakati wengine wamekuwa wakipewa nafasi kufuatana na mahitaji ya mchezo
ADVERTISE HERE