Yanga yapania alama tatu za Mtibwa Sugar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Apr 2019
Yanga yapania alama tatu za Mtibwa Sugar

Vinara wa ligi kuu Yanga wako mkoani Morogoro ambapo leo saa nane mchana watashuka uwanja wa Jamhuri kuikabili Mtibwa Sugar

Baada ya kuzoa alama zote sita kwenye michezo miwili iliyochezwa uwanja wa nyumbani CCM Kirumba, Yanga inasaka alama nyingine tatu ugenini ili kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi wakati huu wa lala salama

Vijana wa kocha Mwinyi Zahera walifanya mazoezi ya mwisho jana kuelekea mchezo huo ambao muda wa kuanza ulibadilishwa ili kuwapa nafasi mashabiki kushuhudia mchezo wa AFCON U17 kati ya Tanzania dhidi ya Uganda utakaopigwa saa kumi jioni

Zahera amesema kikosi chake kiko katika kiwango bora na anaamini wana nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo

Katika mchezo wa leo Yanga itamtegemea kinara wake wa mabao Heritier Makambo ambaye amefunga mabao matatu kwenye michezo miwili iliyopita

Aidha kurejea kwa nahodha Ibrahim Ajib ni habari njema kwa Yanga ambayo itawakosa baadhi ya nyota wake Kelvin Yondani na Feisal Salum wanaotumikia adhabu za kadi nyekundu na njano

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
43m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’