Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito ya Yanga Lucas Mashauri ambaye pia alikuwa akiwania nafasi ya Mwenyekiti kwenye kinyan'ganyiro cha uchaguzi wa Yanga utakaofanyika May 05, amejiondoa katika kinyan'ganyiro hicho
Mashauri ametangaza uamuzi huo mapema leo ambapo amesema baada ya kufanya kikao na wanafamilia, ameona ni vyema aachane na mpango wa kuwania uongozi
Aidha Mashauri amesema pia kutokana na kukabiliwa na majukumu binafsi, hatakuwa na muda wa kutosha kutimiza majukumu yake ipasavyo
Mashauri amebainisha kuwa hata fomu hakuchukua yeye mwenyewe, ni wanachama wa Yanga waliomchukulia wakiamini ana sifa licha ya yeye kuwa safarini
Baada ya kujitoa Mashauri, wagombea waliobaki kuwania nafasi ya Mwenyekiti ni Dk Mshindo Msola na Elias Mwanjala ambao baada ya mchujo wataungana na Dk Jonas Tiboroha na Baraka Igangula waliopitishwa kwenye mchakato wa awali wa kuwania nafasi zilizowazi
Katika hatua nyingine, wagombea sita wa nafasi mbalimbali za uongozi Yanga wamewekewa mapingamizi
Wagombea hao ni pamoja na waliokuwa kwenye Kamati ya Utendaji katika uongozi uliopita ambao walijiuzulu nafasi zao ambao ni Hussein Nyika, Thobias Lingalangala, Samwel Lukumay na Siza Lymo. Wengine ni Elias Mwanjala na Palina Conradi.
Uzoefu na suala la maadili zimetajwa kuwa sababu za mapingamizi hayo.
Aidha, waliokuwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji uongozi uliopita wamewekewa pingamizi wakidaiwa kutowasilisha bajeti ya mapato na matumizi wakati walipokuwa viongozi