Baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda ambaye ni shabiki kindakindaki wa Simba kubeza zoezi la michango linaloendeshwa na klabu ya Yanga, Katibu wa Kamati Maalum ya Uhamasishaji Deo Mutta amewataka Wanayanga wasiumizwe na wanaowabeza na badala yake waendelee kuchangia kwani zoezi hilo limekuwa na mafanikio
Aidha Mutta amebainisha kuwa Kamati itafanya tukio kubwa jijini Dar es salaam kama lililofanyika mkoani Dodoma ambalo litaitikisa NCHI

Jana Makonda alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa Yanga haikupata kitu mkoani Dodoma ukiondoa mchango wa Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa aliyechangia Tsh Milioni moja.
Alisema michango iliyokusanywa Dodoma haizidi laki nne na akawashauri viongozi wa Kamati ya Uhamasishaji kufanya zoezi hilo kwenye mkoa wake wa Dar es salaam kuwa wanaweza wakapata fedha