Zahera ataka alama tatu za Mtibwa Sugar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Apr 2019
Zahera ataka alama tatu za Mtibwa Sugar

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema wamejiandaa kikamilifu kupata ushindi kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar hapo kesho utakaopigwa katika uwanja wa Jamhuri

Zahera amesema Yanga bado iko kwenye mbio za kuwania ubingwa hivyo malengo yao ni kushinda michezo yote iliyobaki

Kocha huyo msaidizi wa timu ya Taifa ya DR Congo amesema haoni timu ya kuizuia Yanga isipate matokeo kwenye michezo iliyobaki

"Sijaona timu ambayo inaweza kutusumbua kama wachezaji wangu watafanya kile ninachowaelekeza, hakuna mechi ngumu, ila kuna ushindani kwenye ligi, tumefaulu kwa kushinda mechi zilizopita, na zilizoko mbele yetu pia tutahakikisha tunashinda, hayo ndiyo malengo yetu," amesema Zahera

Kikosi cha Yanga kiko mkoani Morogoro tangu jana ambapo leo wanatarajia kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Jamhuri ambao utatumika katika mchezo huo

Kesho Yanga huenda ikaongozwa na nahodha wake Ibrahim Ajib aliyerejea kikosini baada ya kupona majeraha ya nyonga

Yanga imepania kushinda mchezo wa kesho ili kuendelea kujikita kileleni kabla ya mchezo dhidi ya Azam Fc utakaopigwa April 29

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’