Keshokutwa Jumatano April 17 Yanga itakuwa uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kupepetana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara
Habari njema kwa Yanga ni kurejea kikosini kwa nahodha wake Ibrahim Ajib aliyeanza mazoezi baada ya kupona majeraha ya nyonga
Aidha baada ya mkongwe Kelvin Yondani kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar, beki kisiki Abdallah Shaibu 'Ninja' aliyemaliza adhabu hivi karibuni, naye amerejea kikosini kuziba pengo lake
Yondani anatarajiwa kukosa michezo mitatu
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kutimkia mkoani Morogoro leo tayari kwa mchezo huo ambao Yanga itaingia ikiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi ambao ulizikutanisha timu hizo mwaka jana
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema lengo lao ni kushinda michezo yote saba iliyobaki ili wajiweke katika nafasi ya kutwaa ubingwa huku wakiomba Simba idondoshe pointi kwenye michezo 12 ya viporo