Kikosi cha Yanga kikiwa na wachezaji 26 na viongozi 12, miongoni mwao 8 wakiwa benchi la Ufundi, kimeondoka leo kuelekea mkoani Njombe tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Njombe Mji, mchezo utakaopigwa Jumapili, Septemba 10 katika dimba la Sabasaba.
Orodha ya wachezaji ni ileile iliyotolewa na uongozi jana ambapo ni wachezaji watatu pekee walioachwa kwenye safari hiyo kutokana na kuwa majeruhi.

Wachezaji hao ni Amissi Tambwe, Benno Kakolanya na Baruani Akilimali.
Baada ya mchezo dhidi ya Njombe Mji, kikosi hicho kitaelekea mkoani Songea kucheza mchezo mwingine dhidi ya Majimaji Septemba 16.

ADVERTISE HERE