Uongozi wa Yanga umewataka wamiliki wa gazeti la Championi kuacha kuandika habari za kutunga, zisizo na ukweli wowote zenye lengo la kuvuruga mipango ya klabu
Katika matoleo ya hivi karibuni, gazeti hilo limeripoti habari za upotoshaji kuhusu zoezi la uchangiaji Yanga likidai klabu hiyo kupokea mamilioni ya fedha kutoka Marekani na nchi za Ulaya
Taarifa iliyotolewa na Yanga katika ukurasa rasmi wa mtandao wa Instagram imebainisha kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na chombo hicho cha habari kinajiaibisha kwa kuandika habari za uongo


ADVERTISE HERE