Waziri Mkuu aichangia Yanga Milioni moja, kupewa cheti Maalum

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Apr 2019
Waziri Mkuu aichangia Yanga Milioni moja, kupewa cheti Maalum

KAMATI YA HAMASA YA KUCHANGIA YANGA 2019

Kamati ya Hamasa ya Kuchangia Klabu ya Yanga inatoa shukurani kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa (MB) Kwa kuwa mchangiaji wa Kwanza kuichangia Klabu ya Yanga ambayo ina historia kubwa ya upatikanaji wa Uhuru wa Nchi yetu ya Tanzania.

Waziri Mkuu ameichangia Klabu ya Yanga kiasi cha shilingi milioni moja (1,000,000/=).

Kamati ya Hamasa kwa niaba ya Wanachama, Mashabiki na Wapenzi wa Klabu ya Yanga ina imani kubwa kuwa, mchango huu utakuwa chachu kwa Viongozi wengine wa ngazi zote kwa Taasisi za Umma na Binafsi bila kujali Itikadi, Jinsia na hata Ushabiki wa kijadi wa Yanga na Simba na hatimaye kuunga mkono jitihada hizi za Kiukombozi za KLABU YA YANGA zenye kauli mbiu ya Timu ya Wananchi Wawekezaji ni Wananchi Wenyewe

Cheti Maalumu kitatolewa kwa Mh. Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Kamati Mh. Anthony Peter Mavunde (MB) wakati wa kuhitimisha zoezi hili Maalumu

Deo Mutta
KNY - Kamati ya Hamasa ya Kuchangia

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’