Winga wa Yanga Juma Mahadhi ameshindwa kurejea dimbani msimu huu kutokana na majeraha makubwa ya goti aliyopata mwanzoni mwa msimu
Mahadhi aliumia August 21 2018 katika mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo ambao Yanga ilishinda 2-1, Mahadhi aliingia mwanzoni mwa kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Pius Buswita, lakini akaumia na kushindwa kuendelea na mchezo nafasi yake ikachukuliwa na Ibrahim Ajib.
Mahadhi alifanyiwa upasuaji wa goti mara mbili na sasa ameendelea kufanya mazoezi maalum ili kuweza kupona kabisa kabla ya kurejea dimbani
Amewashukuru wadau wa klabu ya Yanga kwa sapoti ambayo wameendelea kumpa wakati wote ambao yuko nje ya uwanja akiuguza majeraha
Ameahidi msimu ujao atarejea dimbani akiwa imara