Yanga yasaka alama tatu dhidi ya Kagera Sugar leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Apr 2019
Yanga yasaka alama tatu dhidi ya Kagera Sugar leo

Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga leo wako dimbani uwanja wa CCM Kirumba kuikabili Kagera Sugar katika mchezo wa raundi ya 31

Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya African Lyon juzi, Yanga imepania kuendeleza wimbi la ushindi ili kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi

Kocha Mwinyi Zahera amesema wamefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huo na ana matumaini vijana wake wataibuka na ushindi

"Mchezo dhidi ya Kagera Sugar utakuwa wa nguvu kuliko mchezo tuliocheza na African Lyon," amesema Zahera

"Nimewapa wachezaji mazoezi maalum ili kuwaondolea uchovu uliotokana na safari na kucheza mfululizo"

"Malengo yetu ni kushinda michezo yote iliyobaki, bado nafasi ya kuchukua ubingwa tunayo"

Yanga imejikusanyia alama 71 baada ya kushuka dimbani mara 30. Inaongoza ligi kwa tofauti ya alama nane dhidi ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 63

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’