Baada ya hafla ya uzinduzi wa kuchangia Yanga iliyofanyika mkoani Dodoma jana, Wajumbe wa Kamati Maalum tayari wameondoka Dodoma kurejea jijini Dar es salaam ambako watatoa taarifa na tathmini ya zoezi hilo
Katibu wa kamati hiyo Deo Mutta ametoa shukrani kwa wadau wote wa klabu ya Yanga kwa ushirikiano waliotoa ambapo amesema mpaka sasa wamefanikiwa kwa asilimia 90 kufikia malengo waliyokuwa wamejiwekea
"Kwa niaba ya Wanakamati tunawashukuru wanayanga wote kwa ushirikiano wenu kwa tukio la Uzinduzi wa Zoezi la Hamasa ya Kuichangia timu yetu kwa MAFANIKIO MAKUBWA SANA," imesema taarifa ya Mutta
"Sisi tunajiandaa kuondoka Dodoma kurejea Dar es Salaam. Kifupi ni Kwamba Tumefanikiwa kwa kile tulichokusudia kwa asilimia takriban 90% kwa yale Malengo ambayo Kamati ilijiwekea. TAARIFA KAMILI itawasilishwa mara tutakapofika Dar es Salaam ila TUMEFANIKIWA"
Kamati hiyo ilijiwekea malengo ya kukusanya angalau Tsh Bilioni 1.5, hii ni habari njema kwa Wanayanga ambao hata hivyo wameaswa kuendelea kuchangia
Bado kadi ambazo kila moja ina thamani ya Tsh Milioni moja zimeendelea kugawiwa kwa matawi ya klabu ya Yanga na wadau mbalimbali kote nchini
Wakati kamati hiyo ikiwa safarini kurejea jijini Dar es salaam imeendelea kupokea 'order' za kadi kutoka kwa wadau
Mkoa wa Manyara umepatiwa kadi 10 ambapo kiasi cha Tsh Milioni 10 zitakusanywa kutokana na kadi hizo
Pia matawi matatu ya klabu ya Yanga mkoani Morogoro ymepatiwa kadi tatu mapema leo
Zoezi hilo litafanyika mkoa kwa mkoa ili kuhakikisha msimu wote ujao, Yanga inajiendesha bila ya kutegemea fedha za tajiri mmoja