Tuliache benchi la ufundi lifanye kazi kwa weledi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Sep 2017
Tuliache benchi la ufundi lifanye kazi kwa weledi
Obrey Chirwa amekuwa majeruhi kwa zaidi ya mwezi mmoja. Chirwa aliumia sambamba na Mwashiuya wakati Yanga ikiwa mkoani Morogoro.

Wachezaji wote hawa hawakuwemo kwenye kikosi cha Yanga kilichoweka kambi Pemba na baadae kuivaa Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii.

Tumetaarifiwa wiki hii walianza mazoezi mepesi hivyo benchi la ufundi ndilo linalofahamu ni wakati gani sahihi wa kuanza kuwatumia.

Amissi Tambwe yeye ni kama ana tatizo sugu la goti. Tambwe aliumia siku moja kabla ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

Msimu ulipita Tambwe alipata tatizo kama hili. Naamini madaktari wa Yanga wataweza kumsaidia na majeraha hayo ya mara kwa mara.

Lakini ifahamike matibabu ya majeraha ya goti yanahitaji muda kupona kabisa.

Msimu uliopita Donald Ngoma hakutumika kabisa kwenye mzunguuko wa pili wa VPL. Lakini alipokwenda kutibiwa Afrika Kusini alitakiwa kukaa nje kwa miezi minne.

Leo hii amerejea na tutamuona yuko fiti kabisa.

Madhara ya kumtumia mchezaji ambaye hajapona vizuri majeraha yake ni makubwa zaidi. Anaweza akaumia tena na ikalazimu kuanza tena upya matibabu yake ambayo pia yanaweza yakachukua muda mrefu zaidi.

Kwa mtazamo wangu naona ni vyema benchi la ufundi liachwe lifanye kazi kwa weledi na sio kufuata kelele za mashabiki.

Uvumi kwamba wachezaji hawa wamegoma kucheza eti hawajalipwa mishahara sidhani kama kuna ukweli wowote.

Ilikuwa hivyo kwa Ngoma msimu uliopita lakini leo hii amepona hatusikii tena hizo kelele.

Benchi la ufundi linatakiwa lijenge kikosi imara kwa kuwatumia wachezaji waliopo kikosini sasa. Majeruhi kwenye timu ni jambo la kawaida na hutokea wakati wowote.

Tayari tumesikia kocha George Lwandamina ameuambia uongozi wa Yanga umtafutie mtaalamu mwingine atakayeweza kusaidiana na Daktari wa timu kushughulikia majeraha ya mara kwa mara ambayo yanafanana kwa karibu wachezaji wote ambao ni majeruhi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
59m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’