Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka kesho Ijumaa kuelekea mkoani Njombe kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mji ya mkoani humo mchezo utakaofanyika Jumapili, Septemba, 10.
Wakati kikosi hicho kikitarajiwa kuondoka hiyo kesho bado hakuna uhakika kama Amissi Tambwe ataweza kusafiri licha ya kuanza mazoezi mepesi.
Kocha George Lwandamina alimuondoa Tambwe kwenye program yake ya kikosi kinachotarajiwa kuivaa Njombe Mji.
Wachezaji Amissi Tambwe, Obrey Chirwa na Geofrey Mwashiuya wametoka kwenye majeruhi na huenda wanahitaji muda zaidi wa kuwa fiti.
Ifahamike daktari wa timu ndiye anayetoa idhini ya lini mchezaji aliyekuwa majeruhi aanze kutumika.
Ni dhahiri Lwandamina yuko kwenye presha na atahitaji kupata matokeo katika mchezo huo ili kuweka mambo sawa.
Yanga imeshindwa kupata ushindi kwenye michezo miwili iliyopita dhidi ya Simba na Lipuli.
Kama bingwa mtetezi ni wazi matokeo hayo hayawezi kufurahiwa na mashabiki wa Yanga ambao wamezoea kuiona timu yao ikitoa vipigo.
Matokeo tofauti na ushindi dhidi ya Njombe huenda yakaweka hatarini kibarua cha kocha George Lwandamina.

ADVERTISE HERE