Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Emmanuel Amunike amemwagia sifa kiungo wa Yanga Feisal Salum kuwa anao uwezo wa kucheza soka barani Ulaya
Amunike amesema kiungo huyo anahitaji kuongezewa vitu vichache ili awe bora zaidi
"Kama Feisal angekuwa Ulaya leo basi angekuwa akicheza klabu ya Fc Barcelona," amesema Amunike
"Kwa sababu ubora alionao ni wachezaji wachache sana ambao wanaweza kumfikia"
"Nimemtazama kiufundi zaidi na nimebaini ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa sana"
"Anatakiwa kuimarishwa kidogo tu kiufundi ili mchango wake uwe na manufaa"
Amunike amewahi kuchezea klabu ya FC Barcelona, hivyo anachokizungumza kinatokana na uzoefu wake
Β
Β
ADVERTISE HERE