Nahodha wa kikosi cha Yanga Ibrahim Ajib atakosa mchezo dhidi ya Ndanda Fc utakaopigwa mkoani Mtwara siku ya Alhamisi kutokana na kuwa bado anasumbuliwa na maumivu ya misuli
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema Ajib hatakuwemo kwenye kikosi kinachotarajiwa kuondoka kesho Jumanne kuelekea Mtwara
Aidha nahodha msaidizi Juma Abdul amepona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua na huenda akajumuishwa katika msafara huo
Msafara wa wachezaji 20 na viongozi nane wataondoka kesho asubuhi kwa usafiri wa Ndege
ADVERTISE HERE