Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Malangwe Mchungahela amesema uchaguzi Mkuu wa Yanga utafanyika May 05 badala ya April 28 tarehe iliyokuwa imependekezwa na Bodi ya Wadhamini ya Yanga kwa kuwa siku hiyo itakuwa fainali ya michuano ya vijana ya AFCON
Uchaguzi huo utahusisha nafasi zote za uongozi za klabu hiyo ambapo amefafanua kuwa wagombea waliokuwa wamepitishwa kuwania kujaza nafasi zilizowazi, wataingia moja kwa moja katika kinyan'ganyiro hicho bila kujaza fomu tena
Wagombea hao wataungana na wagombea wengine wakati zoezi la kampeni litakapoanza
Fomu zinaanza kutolewa kesho Makao Mkuu ya klabu ya Yanga
Nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe nane wa Kamati ya Utendaji
Ratiba kamili ya uchaguzi wa Yanga
Aprili 2-7 kuchukua fomu
Aprili 9 Kikao cha mchujo kwa wagombea
Aprili 10 kubandikwa kwa majina yaliyopitishwa
Aprili 11-14 Pingamizi kwa wagombea
Aprili 16-18 Kupitia pingamizi na usaili
Aprili 18-23 Sekretariati kusikiliza maamuzi ya kamati ya maadili
Aprili 24-26 Kukata rufaa
Aprili 27-29 kusikiliza rufaa
Aprili 30- Mei 4 Kampeni
Mei 5 uchaguzi mkuu.