Kamati Maalum ya uchaguzi Yanga imetangaza kuanza kwa mchakato wa uchaguzi kwa kuwaalika wagombea wa nafasi mbalimbali kujitokeza kuchukua fomu.
Fomu za kuwania nafasi za uongozi katika klabu ya Yanga zitaanza kutolewa kesho April 02 2019 Makao Makuu ya klabu ya Yanga Mtaa wa Twiga na Jangwani jijini Dar es salaam
April 07 ndio siku ya mwisho ya zoezi la utolewaji wa fomu.
Nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, na Wajumbe nane wa kamati ya utendaji. Uchaguzi utafanyika May 05 2019
ADVERTISE HERE