Baada ya juzi kukata tiketi ya kutinga nusu fainali ya kombe la FA, kikosi cha Yanga leo kimerejea mazoezini kujiandaa na mchezo unaofuata ambao ni wa ligi kuu dhidi ya Ndanda Fc
Mchezo huo utapigwa Alhamisi, April 04 mkoani Mtwara kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona
Yanga ilirejea jijini Dar es salaam kutoka Mwanza jana ambapo kocha Mwinyi Zahera aliwapa wachezaji mapumziko ya siku moja
Mabingwa hao wa kihistoria Tanzania, wako kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa wamejikusanyia alama 67 wakifuatiwa na Azam Fc (59) na Simba (57)
Ndanda Fc ilifanikiwa kuwalazimisha sare ya bao 1-1 vinara hao wa ligi katika mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa
Kikosi cha Yanga kitaelekea mkoani Mtwara kesho Jumanne tayari kwa mchezo huo
ADVERTISE HERE