Penati ya Ngasa yasababisha simanzi Kilosa, yaua shabiki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Apr 2019
Penati ya Ngasa yasababisha simanzi Kilosa, yaua shabiki

Juzi katika mchezo wa robo fainali ya kombe la FA kati ya Alliance Fc dhidi ya Yanga, winga Mrisho Ngasa na Kelvin Yondani walikosa mikwaju ya penati licha ya Yanga kushinda kwa penati 4-3

Penati ya Ngasa imesababisha simanzi wilayani Kilosa baada ya kusababisha kifo cha shabiki wa Yanga aliyefahamika kwa jina la Magambo M. Magambo

Kwa mujibu wa Sport Xtra, shabiki huyo alifariki akiwa anaangalia mpira kwenye 'kibandaumiza' pamoja na watazamaji wengine.

"Nilimpokea ndugu yangu hapa Kilosa tarehe 21 mwezi huu (3) akitokea Mwanza ambako ndipo alikuwa anaishi, anaitwa Magambo M. Magambo ana miaka 48. anasema Peter Lutandula ndugu wa karibu wa marehem."

"Jana tulitoka kwenda kibandani kuangalia mechi ya Alliance na Yanga, baada ya Mrisho Ngasa kukosa penati (penati za kutafuta mshindi) ndugu yangu akashtuka akafanya aaah! akaanguka na kupoteza maisha."

"Juhudi za kumsaidia zilishindikana tukapiga simu polisi wakaja tukaenda kuripoti kituo cha polisi baadaye tukaruhusiwa kuendelea na taratibu nyingine."

"Marehemu ni shabiki wa Yanga, alikuwa ni mpenzi wa Yanga kwelikweli lakini siwezi kusema kama alikuwa anatatizo la afya kwa sababu mwili wa mtu anaujua mwenyewe"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’