Uwanja wa Uhuru ulikuwa wa kwanza kufungwa kabla ya viwanja vya Taifa na Azam Complex kupisha ukarabati tayari kutumika kwenye michuano ya AFCON U17 inayotarajiwa kutimua vumbi jijini Dar es salaam kuanzia April 14-28 2019
Ukarabati wa uwanja wa Uhuru uko katika hatua za mwisho kukamilika ambapo tayari uwanja huo umetandikwa nyasi bandia mpya
Kulingana na taarifa iliyotolewa na TFF, uwanja wa Uhuru utatumika kwa ajili ya mazoezi kwa timu zitakazoshiriki michuano hiyo ya AFCON ya vijana huku viwanja vya Taifa na Azam Complex vikitumika katika mashindano
ADVERTISE HERE