Yanga inatarajiwa kushuka dimbani Jumapili ijayo, Septemba 10 kucheza mchezo wa pili wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Njombe Mji.
Mchezo huo wa ugenini utapigwa kwenye dimba la Sabasaba mkoani Njombe kuanzia saa kumi kamili jioni.
Sasa kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amesema timu yake imajipanga kuibuka na ushindi katika mchezo huo.
Amesema ushindi mnono itakayopata Yanga kwenye mchezo huo itakuwa salamu kwa timu nyingine kwamba sasa ndiyo Yanga imeanza ligi rasmi.
"Najua msimu huu kila timu imejipanga kuhakikisha inafanya vizuri, hivyo basi baada ya kuona tumetoka sare mechi ya kwanza, tumejipanga kushinda mechi ijayo ili kudhihirisha ubora wetu ambao tuliokuwa nao msimu uliopita mpaka tukawa mabingwa", amefunguka Lwandamina
"Tunataka kutetea taji letu na safari ya kufanya hivyo tunaianzia Njombe, baada ya hapo mambo yote nadhani yatakaa sawa, tunataka kushinda kila mechi iliyo mbele yetu ili kutetea taji letu."
Yanga ilianza kwa kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Lipuli, timu iliyopanda daraja msimu uliopita sambamba na Njombe Mji na Singida United.

ADVERTISE HERE