Tanzania, Uganda, Kenya, Burundi zapongezwa kutinga AFCON 2019

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Mar 2019
Tanzania, Uganda, Kenya, Burundi zapongezwa kutinga AFCON 2019

Baraza la Vyama Vya Michezo wa Mpira wa Miguu la Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) limezipongeza timu nne za ukanda wake kwa kufuzu fainali za mashindano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) yaliyopangwa kufanyika nchini Misri mwezi Juni na Julai.

Tanzania, Uganda, Kenya na Burundi zimefanikiwa kufuzu katika fainali hizo zilizopangwa kuanza Juni 21 mpaka Julai 19 mjini Cairo.

Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alisema kuwa kitendo cha kuingiza timu nyingi katika mashindano makubwa ya Mataifa ya Afrika ni ushahidi tosha kuwa soka la ukanda wa Cecafa linazidi kupata maendeleo makubwa na kuomba nchi ambazo hazijafikia hatua hiyo kujitahidi.

"Kwa kweli hii ni sifa kubwa kwa Cecafa na heshima kwa mchezo kwa ujumla. Ni miaka mingi hatujawahi kupata timu nyingi katika mashindano makubwa ya Afrika, kwa kweli in ni faraja kwetu," alisema Musonye.

Musonye amesema kuwa ni wakati wa kuanza maandalizi ya fainali za Afcon ambazo ni mashindano magumu kutokana na kushirikisha timu magwiji ya soka ya bara la Afrika.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’