Samatta kuongoza kikosi cha ushindi Stars

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Mar 2019
Samatta kuongoza kikosi cha ushindi Stars

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mbwana Samatta kesho Jumapili atabeba matumaini ya Watanzania kuelekea fainali za AFCON 2019 atakapokiongoza kikosi cha Stars katika mchezo dhidi ya Uganda Cranes

Samatta, kinara wa mabao ligi kuu ya Ubelgiji, amewatoa hofu Watanzania kuelekea mchezo huo akiahidi kuwa watafanya kile walichoelekezwa na Kocha Emmanuel Amunike ili waweze kuibuka na ushindi

"Tumefanya maandalizi ya kutosha. Tunafahamu mchezo hautakuwa mwepesi lakini tunayo kila sababu ya kutumia vyema uwanja wetu wa nyumbani kupata ushindi," amesema Samatta

Matokeo ya ushindi dhidi ya Uganda yanaweza kuipa Stars nafasi ya kufuzu kwa fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika mwezi Juni nchini Misri.

Hata hivyo ili Stars iweze kufuzu lazima Cape Verde iifunge au itoke sare na Lesotho. Mchezo baina ya timu hizo utapigwa huko Cape Verde muda sawa na mchezo kati ya Stars dhidi ya Uganda utakaopigwa saa 12 jioni

Wapinzani wa Stars, Uganda Cranes wanatarajiwa kuwasili nchini leo

Uganda iliweka kambi ya wiki moja nchini Misri kujiandaa na mchezo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’