Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh Jokate Mwegelo ambaye ni Mjumbe wa Kamati Maalum ya Uhamasishaji, amewataka wapenzi, wanachama na mashabiki wa klabu ya Yanga kuendelea kuichangia timu ili iweze kupata nguvu ya kukiboresha kikosi kwa ajili ya msimu ujao
Yanga kupitia Kamati hiyo Maalum inayoongozwa na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mh Anthony Mavunde, imedhamiria kukusanya angalau Bil 1.5 ili kuweza kufanikisha azma ya kocha Mwinyi Zahera aliyehitaji angalau Bil 2 kwa ajili ya usajili pamoja na kulipa mishahara ya wachezaji

Mh Mwegelo ameungana na Wajumbe wengine wa Kamati Maalum kuwahamasisha Wanajangwani waendelee kuichangia timu yao


ADVERTISE HERE