Amunike apania kuvunja rekodi ya Stars mwaka 1980

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Mar 2019
Amunike apania kuvunja rekodi ya Stars mwaka 1980

Jumapili timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itakuwa ikisaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019 itakapochuana na Uganda Cranes

Stars inayonolewa na kocha Emmanuel Amunike, ilishiriki kwa mara ya mwisho fainali za michuano hiyo mwaka 1980 wakati huo ikiwa chini ya Mpoland Slowmir Work aliyesaidiwa na wazalendo marehemu Joel Bendera na Ray Gama

Ni miaka 39 imepita tangu Stars ishiriki fainali za michuano hivyo kuna kila sababu Watanzania 'kuupania' mchezo wa Jumapili kwani huenda historia mpya itaandikwa

JINSI ILIVYOFUZU MWAKA 1980

Stars wakati huo ikiwa chini ya Kocha, Slowmir Work kutoka Poland, akisaidiwa na Joel Bendera na Ray Gama, ilikata tiketi ya kushiriki Fainali hizo za Afrika ambazo sasa kila mmoja ana kiu ya kuona Tanzania kwenye luninga ikicheza kwa mara nyingine.

Novemba 11,1979 Stars ilikwenda Zambia kurudiana na 'KK Eleven', kikosi cha timu ya Taifa ya Zambia baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa jijini Dar es salaam.

Bao la ushindi kwa upande wa Stars katika mchezo wa kwanza lilifungwa na kiungo, Mohammed Rishard Adolph ambaye sasa ni kocha wa Tanzania Prisons

Katika pambano hilo lililochezwa mjini Ndola, nje kidogo ya jiji la Lusaka, Taifa Stars ilikuwa ikihitaji sare ya aina yoyote ili ifuzu fainali hizo kwa mara ya kwanza tangu ilipoanza kushiriki mwaka 1968.

Katika mchezo huo wa marudiano, 'KK Eleven' walipata bao la mapema ambalo lilidumu hadi dakika ya 85.

Dakika tano za mwisho, mshambuliaji wa Pan African wakati huo, Peter Tino alibadili sura ya mchezo kwa kusawazisha bao na kunyamazisha umati wa mashabiki waliofurika kwenye Uwanja wa Ndola.

ilipigwa kona kuelekezwa lango la Stars, lakini kipa wake, Juma Pondamali β€˜Mensar’ akaupangua kwa ngumi, ukamkuta kiungo Leodegar Tenga ambaye naye alitoa pasi ndefu kwa Hussein Ngulungu aliyemgongea pasi ndefu Tino aliyeukwamisha kimiani.

Tino aliwatoka mabeki wa Zambia na alipofika nje kidogo ya eneo la hatari la Zambia, alitandika kombora la mguu wa kulia, lililompita kipa wa Zambia aliyekuwa kikwazo, John Shileshi.

Katika mchezo ule Tanzania iliwakilishwa na Juma Pondamali aliyekuwa langoni, Leopard Tasso, Mohammed Kajole/ Ahmed Amasha, Salim Amir, Jella Mtagwa, Leodegar Tenga, Hussein Ngulungu, Omari Hussein, Peter Tino, Mohamed Salim na Thuweni Ally.

FAINALI ZA LAGOS

Katika fainali hizo, Taifa Stars ilichapwa mabao 3-1 na wenyeji Nigeria katika mechi ya ufunguzi, ikatoka sare ya mabao 2-2 na Ivory Coast kabla ya kuchapwa mabao 2-1 na Misri na kutolewa hatua ya makundi.

Historia hii inaweza ikajirudia keshokutwa Jumapili kama Stars itafanikiwa kupata ushindi dhidi ya Uganda na Cape Verde ikaichapa au kutoka sare ya Lesotho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’