Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa robo fainali kombe la FA (ASFC) dhidi ya Alliance Fc
Yanga inajifua chini ya kocha Msaidizi Noel Mwandila anayetekeleza majukumu hayo kwa niaba ya kocha Mwinyi Zahera ambaye yuko Congo DR akikabiliwa na majukumu ya kikosi cha timu ya Taifa
Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema hakuna majeruhi wapya, beki Andrew Vicent Chikupe ni mchezaji pekee anayekosekana kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli
Chukupe huenda akaukosa mchezo dhidi ya Alliance utakaopigwa jijini Mwanza Jumamosi ya March 30 2019
ADVERTISE HERE