Chonde chonde Bodi ya ligi msibadili tena ratiba - Chicharito

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Sep 2017
Chonde chonde Bodi ya ligi msibadili tena ratiba - Chicharito
Kaimu Afisa Habari wa Yanga Godlisten Anderson 'Chicharito' amaiomba bodi ya Ligi kukahikisha ratiba inaendelea kubaki kama ilivyo ili isije kuwaumiza wachezaji kisaikolojia.

Chicharito ameeleza leo ikiwa zimebakia siku chache kuelekea mchezo wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa Septemba 10 katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe na kusema hawawezi kubishana na wapanga ratiba ila wanavyokuwa wanabadilisha mara kwa mara wanawatoa wachezaji katika molali ya mchezo.

"Kikawaida hatuwezi kubisha kwa sababu ratiba imeshatoka kikubwa ni kuifuata kama ilivyopangwa lakini tunawaomba wapangaji wa ratiba wajitahidi iendelee kubakia kama ilivyo isiwe na mabadiliko ya kila mara", amesema Chicharito.

Pamoja na hayo, Chicharito amesema mpaka hivi sasa wachezaji wake wote wanaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo dhidi ya Njombe Mji FC.

"Kikosi bado kinaendelea na mazoezi yake katika uwanja wa Uhuru, kuhusu suala la safari tutatoa taarifa maalumu kwamba itakuwa siku gani kwa sababu tumeambiwa mechi itakuwa siku ya Jumapili", amesisitiza Chicharito.

Kwa upande mwingine, Chicharito amesema kwa mujibu wa taarifa alizozipokea kwa daktari wa timu hiyo ni kuwa wachezaji majeruhi wameshaanza mazoezi mepesi ya kuweka mwili sawa kuanzia siku ya jana ili waweze kujiunga na wenzao.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’