Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaya amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kuiunga mkono Taifa Stars itakapochuana na Uganda Cranes Jumapili March 24 katika mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019
Kaya amesema ni muhimu kwa mashabiki wote wa soka nchini kuweka kando vilabu vyao na kuiunga mkono Stars kwa umoja wao
"Timu ya Taifa ni yetu sote, tuachane na mambo ya kusema timu hii sijui imejaa wachezaji wa timu fulani. Tuiunge mkono kwani ushindi wa Stars ni ushindi wetu sote," amesema
"Tujenge utamaduni wa kuweka tofauti zetu za vilabu kando kwa kuziunga mkono timu zinazokuwa zinawakilishi Taifa letu"
Stars inahitaji kushinda mchezo wa Jumapili ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kwa fainali za AFCON 2019
Watanzania wamehamasishwa kujitokeza kwa wingi uwanjani lengo likiwa kuujaza uwanja wa Taifa unaochukua mashabiki takribani elfu 60
Kiingilio cha mchezo huo ni Tsh 2000/- tu