Licha ya kuanza mazoezi mepesi jana, washambuliaji Obrey Chirwa na Amissi Tambwe hawataweza kusafiri na kikosi cha Yanga kinachoelekea mkoani Njombe kucheza na Mji, Jumapili ijayo, Septemba 10, Imefahamika.
Imeelezwa kuwa Chirwa anahitaji muda zaidi wa mazoezi ili aweze kuwa fiti kutokana na majeruhi yaliyomfanya ashindwe kuitumikia Yanga katika mchezo wowote msimu huu.
Maumivu ya goti yalimuweka Chirwa nje kwa mda mrefu na hata kushindwa kuwemo kwenye kikosi cha Yanga kilichokuwa kimeweka kambi Kisiwani Pemba.
Tambwe naye hatarajiwi kuwa tayari kucheza mchezo huo dhidi ya Njombe.
Wachezaji wengine Beno Kakolanya, Burhani Akilimali na Geofrey Mwashiuya nao licha ya kuanza mazoezi mepesi hawatarajiwi kutumika katika mchezo huo.
Baada ya sare kwenye mchezo wa kwanza, Yanga inahitaji kupata ushindi katika mchezo dhidi ya Mji Njombe ili kuepuka kuvuruga mapema mipango yake ya kutetea ubingwa wa VPL kwa msimu wa nne mfululizo.

ADVERTISE HERE