Baada ya mapumziko ya siku tatu, kikosi cha Yanga leo kimerejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa kombe la FA dhidi ya Alliance Fc
Mchezo huo utapigwa March 30 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
Yanga inajifua chini ya kocha wake msaidizi Noel Mwandila baada ya Mwinyi Zahera kutimkia Congo kutimiza majukumu ya timu ya Taifa
Zahera atarudi baada ya mchezo kati ya Congo DR dhidi ya Liberia utakaopigwa March 24, ukiwa ni mchezo wa mwisho wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019
Β
ADVERTISE HERE