Mlinda lango Klaus Kindoki kwa sasa amejesha makali yake na ameanza kupewa 'heshima' ya kipekee na mashabiki wa klabu ya Yanga ambao mwanzo hawakuwa na imani nae
Hata hivyo Kindoki amesema alilazimika kufanya kazi ya ziada kuweza kurejesha uwezo wake
Kindoki aliyetua Yanga mwanzoni mwa msimu alianza vizuri maisha yake kunako klabu hiyo kwa kufanya vizuri katika michezo ya maandalizi ya msimu
Hata hivyo mambo yalibadilika ligi ilipoanza na kujikuta akifanya makosa ambayo baadae yalionekana kumuondolea kujiamini na kuingia matatani mbele ya mashabiki wa Yanga ambao hawakuwa tayari kumuona akiwa langoni
"Mwenyewe nilikuwa najishangaa kwa nini hali ile ilinitokea," alisema Kindoki katika mahajiano na gazeti la Mwanaspoti
"Hata rafiki zangu pia walishangaa kwani nilianza vizuri lakini kiwango changu kikaanza kushuka ghafla. Wengine walinishauri nitizame upande wa pili kuangalia kama kulikuwa na 'mambo ya gizani'"
"Sikuwa naamini kama hilo lipo ingawa kila nilipokutana na watu, mashabiki na baadhi ya wachezaji walikuwa wananiambia kuna ushirikina nimefanyiwa.
"Kuna mambo ambayo siwezi kuongea kwa vyombo vya habari kuwa walikuwa wanamtaja mtu aliyenifanyia.
"Hilo liliniumiza nikakosa furaha na kazi yangu tatizo nililibaini hapa Tanzania wachezaji wengi ni wazuri lakini wanapenda sana kuendekeza imani za kishirikina," alisema Kindoki.
Kindoki pia alitaja lugha ya kiswahili kuwa kikwazo kingine kilichomfanya ashindwe kufanya vizuri mwanzoni kwani alishindwa kuzungumza na wachezaji wenzie uwanjani
Lakini kwa sasa amejifunza ligha hiyo na anaweza kuwaelekeza wachezaji wenzake hasa mabeki wajipange vipi katika kutimiza majukumu yao ya ulinzi
Kindoki na Kabwili wamekuwa wakipokezana majukumu ya kulinda lango la Yanga baada ya timu hiyo kumsimamisha Beno Kakolanya ameyataka kuvunja mkataba wake ili akajiunge na Simba