Mashabiki wa soka nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa Jumapili wakati kikosi cha Stars kitakapochuana na Uganda Cranes katika mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019
Kupitia Mkutano wake na Waandishi wa Habari jana, Mwenyekiti wa Kamati ya saidia Stars ishinde, Mh Paul Makonda alisema imefika wakati kwa mashabiki wote wa soka nchini kuungana kuiunga mkono tmu ya Taifa ili iweze kufuzu michuano ya AFCON baada ya kusubiri kwa miaka 39
Stars inahitaji kushinda mchezo huo utakaopigwa March 24 ukitarajiwa kuanza saa 12 jioni sambamba na mcheoz mwingine wa kundi L kati ya Cape Verde dhidi ya Lesotho
"Ninawaomba watu wote tujitokeze kuiunga mkono Taifa Stars, tusimame na Stars, tuhakikishe tunaacha tofauti zetu, tuhakikishe kila mmoja anatimiza jukumu lake, tutumie fursa hii kuhakikisha Stars inashinda," alisema Makonda.
"Sisi tunaunganishwa na Taifa Stars, tuitumie Stars kama sehemu ya kutuunganisha, AFCON 2019 ni zamu yetu"
Tayari kikosi cha Stars kimeshaingia kambini kujiwinda na mchezo huo