Uongozi wa klabu ya Yanga umesema umejipanga kukusanya angalau Bilioni 1.5 katika kampeni yake ya uchangiaji wa timu hiyo
Hivi karibuni Yanga ilitangaza kuundwa kwa Kamati ya uhamasishaji wa zoezi hilo, kamati inayoongozwa na Mh Anthony Mavunde
Wajumbe wa Kamati hiyo wamekutana jijini Dar es salaam leo kwenye kikao chao cha kwanza
Mkakati ulioandaliwa na Kamati hiyo ni kuhakikisha malengo ya kukusanya Bil 1.5 yanafanikiwa ambapo zoezi la uchangishaji litaendeshwa mkoa kwa mkoa
Yanga imedhamiria kuboresha kikosi chake mwishoni kwa msimu kwa kutimiza ushauri uliotolewa na kocha Mwinyi Zahera
ADVERTISE HERE