Tanzania kuingiza timu nne michuano ya CAF msimu wa 2020/21

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Apr 2019
Tanzania kuingiza timu nne michuano ya CAF msimu wa 2020/21

Mafanikio ya Simba kwenye Ligi ya Mabingwa, yameinyanyua Tanzania hadi nafasi ya 12, ambayo ndiyo ya mwisho katika orodha ya nchi zinazopewa nafasi nne katika mashindano ya Afrika.

Kabla ya msimu huu, Tanzania ilikuwa nafasi ya 26 na pointi tatu zilizotokana na Yanga kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho, 2016 na 2018.

Kufuzu kwa Simba robo fainali msimu huu, kumeipatia Tanzania pointi 15 ambazo zikichanganywa na zile 3 za Yanga, itafikisha pointi 18

POINTI

CAF hupima viwango vya nchi kupitia mafanikio ya vilabu vyake, kwenye mashindano ya Afrika, kwa kipindi cha miaka mitano.

Viwango vipya vitakavyotoka vikijumuisha mafanikio ya Simba 2018/19, vitaanzia 2015.

Mwaka wa karibuni zaidi huwa na thamani kubwa zaidi (maksi 5) kuliko mwaka wa nyuma zaidi (maksi 1).

Thamani ya mwaka wa mashindano huzidishwa na pointi ambazo klabu huzipata kutokana na mafanikio yake kwenye mashindano husika, na kuwa pointi za nchi.

KOMBE LA SHIRIKISHO

Klabu itakayoshika nafasi ya 4 kwenye makundi, hupewa pointi 0.5. Nafasi ya 3, pointi 1, robo fainali, pointi 2, bingwa pointi 5.

Yanga ilifuzu hatua ya makundi mwaka 2016 na 2018, na kumaliza ya 4 mara zote mbili.

Thamani ya mwaka 2016 ni maksi 2, maana yake ni 0.5 Γ— 2 = 1. Thamani ya mwaka 2018 ni maksi 4, maana yake ni 0.5 Γ— 4 = 2.

Kwa hiyo Tanzania ilivuna pointi tatu kutokana na mafanikio ya Yanga, 2016 na 2018!

LIGI YA MABINGWA

Kufuzu makundi tu ni pointi 0.5 na kufika robo fainali ni pointi 3. Simba imefika robo fainali 2018/19 ambao thamani yake ni maksi 5. Maana yake ni 3X5=15.

Pointi 15 zikijumlishwa na zile tatu za Yanga, Tanzania inakuwa na pointi 18.

Hata hivyo, pointi hizi zitaingia kwenye mahesabu kuanzia msimu ujao kwa ajili ya matumizi ya msimu wa mbele yake, yaani 2020/2021.

Hakuna uwezekano wa pointi ilizofikisha Tanzania kuvukwa na nchi nyingine kwa sababu walio chini hawana timu zilizopo kwenye mashindano ya CAF msimu huu.

Hivyo msimu wa 2020/21 Tanzania itaingiza timu nne mashindano ya vilabu barani Afrika, mbili klabu bingwa na mbili kombe la Shirikisho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’