Mwenyekiti wa Kamati ya Saidi Stars ishinde Mh Paul Makonda leo anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari kuweka hadharani mikakati ya kuipeleka Tanzania kwenye fainali za michuano ya AFCON 2019 itakayofanyika mwezi June nchini Misri

Jumamosi ya wiki hii Stars itashuka dimba la Taifa kuikabili Uganda Cranes katika mchezo ambao ni lazima kwa Tanzania kupata matokeo ya ushindi huku ikiomba Lesotho isipate ushindi ugenini dhidi ya Cape Verde
Stars inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi L linaloongozwa na Uganda ambayo tayari imefuzu baada ya kujikusanyia alama 11
Lesotho inashika nafasi ya pili ikiwa na alama sita, ikifuatiwa na Stars yenye alama tano
Cape Verde iko mkiani ikiwa na alama nne
ADVERTISE HERE