Hesabu kali zinahitajika kombe la FA

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Mar 2019
Hesabu kali zinahitajika kombe la FA

Baada ya kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Lipuli Fc, hatma ya ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga itategemea zaidi na makosa yatakayofanywa na wapinzani wao Simba

Simba ina michezo 11 mkononi na kimahesabu itakuwa na faida ya alama nane zaidi ya Yanga kama itaweza kushinda mcihezo yote

Hata hivyo, Yanga haiwezi kukata tamaa ya ubingwa wakati huu hasa ikizingatiwa iko kileleni mwa msimamo wa ligi.

Simba itahitaji kucheza, kushinda ili iweze kuifikia Yanga ambayo inaongoza kwa tofauti ya alama 16 dhidi yao

Yanga inahitaji kupata nafasi ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao baada ya kukosa mwaka huu

Ukiachana na ubingwa wa ligi kuu, nafasi hiyo pia inaweza kupatikana kama itatwaa taji la kombe la FA

Sasa ikiwa hatua ya robo fainali, imebakisha hatua mbili tu ili iweze kucheza fainali ya michuano hiyo itakayofanyika mwishoni mwa msimu huko Lindi

Mwishoni mwa mwezi huu Yanga itashuka dimba la CCM Kirumba kuikabili Alliance Fc katika mchezo wa robo fainali ya michuano hiyo

Hapa kocha Mwinyi Zahera na benchi lake la ufundi watapaswa kupiga hesabu kali ili kuiwezesha Yanga kupenya kwenye michuano hii ambayo ushindani umezidi kuongezeka

Yanga iliyohamishia makazi yake jijini Mwanza kwa muda, inapaswa kutilia mkazo michuano ya FA ili kujiwekea mazingira mazuri ya kupata tiketi ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’