Ajib mgonjwa, kuikosa Lipuli Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Mar 2019
Ajib mgonjwa, kuikosa Lipuli Fc

Nahodha wa Yanga Ibrahim Ajib ameondolewa katika kikosi kinachosafiri kwenda mkoani Iringa baada ya kuugua

Yanga itaikabili Lipuli Fc bila ya kuwa na mpishi wake huyo wa mabao aliyehusika katika mabao 21 kati ya 45 yaliyofungwa kwenye ligi

Hata hivyo kukosekana kwake hakuwezi kuwa tatizo kwa kikosi cha Mwinyi Zahera kilichosheheni viungo wengi

Mohammed Issa 'Banka', Thabani Kamusoko na Haruna Moshi 'Boban' wote wanaweza kucheza nafasi yake.

Kwa michezo ya hivi karibuni, Ajib amekuwa akitokea benchi kuongeza nguvu kwenye kipindi cha pili

Changamoto pekee inayoikabili Yanga huenda ikabaki kwenye safu ya ulinzi baada ya kukosekana kwa Andrew Vicent ambaye ni majeruhi na Abdallah Shaibu 'Ninja' aliyefungiwa michezo mitatu

Kocha Noel Mwandila huenda akalazimika kumtumia kiraka Said Juma Makapu kwenye nafasi ya ulinzi sambamba na mkongwe Kelvin Yondani.

Pia yupo beki aliyepandishwa kutoka Yanga B Cleosaf Sospeter

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
32m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’