Kabla hajaelekea DR Congo, jana kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera kwa kushirikiana na viongozi wa Yanga waliandaa Semina maalum ya kuwajenga wachezaji kisaikolojia kabla ya timu kuelekea mkoani Iringa kuikabili Lipuli Fc
Zahera na baadhi ya viongozi waandamizi wa Yanga walizungumza na wachezaji katika hafla fupi iliyofanyika jana usiku katika Hoteli ya Nefaland
Zahera amewataka wachezaji wa Yanga wahakikishe wanapambana washinde mchezo huo ili kujiongezea pointi ambazo mwishoni mwa msimu zinaweza kuwasaidia kutwaa ubingwa
Amesema hesabu zao ziwe ni kushinda michezo yote iliyobaki bila ya kuwahofia wapinzani wao ambao wanakutana nao
Yanga inaondoka leo jijini Dar es salaam kuifuata Lipuli Fc tayari kwa mchezo utakaopigwa Jumamosi katika uwanja wa Samora