Misuli inavyomtesa Chikupe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Mar 2019
Misuli inavyomtesa Chikupe

Beki kisiki wa Yanga Andrew Vicent Chikupe huenda akaukosa mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Lipuli Fc kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya misuli

Yanga inaondoka leo kuelekea mkoani Iringa kuifuata Lipuli Fc tayari kwa mchezo huo utakaopigwa keshokutwa Jumamosi kwenye uwanja wa Samora

Yanga inakabiliwa na changamoto katika safu yake ya ulinzi kwani itakosa huduma ya beki Abdallah Shaibu 'Ninja' aliyefungiwa michezo mitatu

Chikupe amekuwa nje ya dimba kwa zaidi ya wiki tatu mara ya mwisho alishiriki mchezo wa kombe la FA (ASFC) dhidi ya Namungo Fc uliofanyika mkoani Lindi

Amejumuishwa katika kikosi cha timu ya Taifa kinachoshuka dimbani March 24 kuikabili Uganda kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019

Kuna uwezekano mdogo kwa beki huyo aliyesajiliwa na Yanga kutoka Mtibwa Sugar kuwa fiti kuweza kucheza mchezo huo

Chikupe amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya misuli mara kwa mara

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’